Thursday , 9th Oct , 2014

Wasanii wanaofanya vizuri katika muziki Uganda, Radio pamoja na Weasel wamerejea kwa kishindo nchini humo baada ya ziara ndefu huko Ulaya na Marekani ambayo imeunyanyua muziki wao kwa kiasi kikubwa.

wasanii wa muziki nchini Uganda Mose Radio na Weasle TV

Radio na Weasel wamekaribishwa na mashabiki wao kupitia sherehe maalum iliyofanyika huko jijini Kampala, ikiambatana na onesho la wasanii hao ambao pia wanatarajiwa kuachia ladha mpya baada ya kuwa bize na ratiba za maonesho.

Kundi hilo pia lina maratajio ya kufanya makubwa zaidi kuelekea mwisho wa mwaka huu, huku likiwa limeongeza nguvu katika sekta ya menejimenti kwa kumuajiri meneja mpya, Lawrence ambaye alikuwa akifanya kazi na Bobi Wine.