
Simba na Yanga
SMG ameyasem hayo mkoani Kigoma baada ya kukamilisha ratiba ya michezo miwili ya kirafiki mkoani humo, ambapo mchezo wa kwanza Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mwamgongo FC na mechi ya pili ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Kigoma United.
Kuelekea pambano dhidi ya watani wao Simba, litakalopigwa Januari 4, 2020, kocha Said Maulid amesema,"Mimi nafikiri mechi za watani hazinipi shida kwa sababu nina uzoefu na mechi za Simba na Yanga. Ni mechi ambazo zina mihemko lakini ni za kawaida sana".
Yanga imeanza kujipanga vyema kuelekea mchezo huo, ikiwa pamoja na kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji kwa kumuongeza Tariq Seif Kiakala kufuatia kuachana na mshambuliaji Juma Balinya.
Pia imemaliza tatizo la mishahara ya wachezaji wake na kufanikiwa kumrejesha mlinzi kisiki, Lamine Moro ambaye awali alitimka klabuni hapo. Kwa upande wa Simba inajiandaa na mechi hiyo baada ya kupata kocha mpya, Sven Vanderbroeck ambaye atakuwa na kazi ngumu katika mchezo huo mkubwa kabisa Afrika Mashariki na Kati.