Monday , 16th Dec , 2019

Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea amesema hakuna uhusiano wowote wa mtu kuwa Mbunge na kupata Kitambi, bali alichoeleza kinachotokea ni mabadiliko ya kawaida ya kimwili.

Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Temeke.

Mtolea ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye Kipindi cha KIKAANGONI, kinachoruka kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana hadi saa 9 : 30 Mchana.

Mtolea amesema kuwa "Kulinganisha vitambi na Ubunge naweza kusema nimeshindwa lakini nachoweza kusema binadamu anabadilika wa mwaka jana hawezi kuwa wa mwaka huu"

"Ila katika muonekano wangu (akionesha kitambi) sijawahi kuamini kuwa unaingiliana kabisa na utekelezaji wa majukumu yangu ya Kibunge" ameongeza Mtolea