Sunday , 15th Dec , 2019

Watu 37 wanatajwa kula Chakula chenye sumyu walipokuwa msibani katika eneo la Mtumba jijini Dodoma, ambapo wote wameshafikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na wanaendelea na matibabu.

Ugali

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma Dkt. Ibenzia Ernest amethibitisha hayo wakati akizungumza na  EATV na EA Radio ambapo tayari timu imeshaenda kwa ajili ya uchunguzi.

"Ni kweli tumepokea watu 37, na tunaendelea na matibabu na walikula hicho chakula jana jioni, na walikula ugali maharage, na uzuri zaidi hakuna taarifa ya kifo." amesema Mganga wa Hospitali ya Dodoma

"Tumeshatuma wataalam ndani ya muda mfupi mtapata majibu." ameongeza Dkt. Ernest