Friday , 30th Aug , 2019

Leo tumepiga stori na msanii wa kike Maua Sama, ambaye ameeleza jambo ambalo hatakuja kulisahu katika maisha yake na 'issue' za kufunga ndoa na mpenzi wake.

Maua Sama

Maua Sama ameileza EATV & EA Radio Digital kuhusu changamoto ambazo anakutana nazo kama mtoto wa kike kwenye muziki.

"Changamoto yangu kubwa ambayo imeniyumbisha katika maisha yangu ni ile ya kukamatwa na polisi kuwekwa mahabusu mwaka jana mwishoni, ilikuwa changamoto kubwa zaidi ikatika maisha yangu iliniumiza na bado inaniumiza ila namshukuru Mungu tupo gado".

Aidha msanii huyo ameendelea kusema ana matukio mengi anayoyakumbuka katika maisha yake ila la kukamatwa ni la kwanza zaidi.

Pia Maua Sama amesema hataki kumuonyesha mpenzi wake kwa sababu mahusiano yake ni mambo binafsi na ndoa yake ikitokea watu wataiona tu.

Licha ya kukaa kwa mwaka mmoja bila kuachia kazi mpya Maua Sama amesema alikuwa  haogopi kuachia kazi kutokana na kuhofia kutotoa wimbo mkali wa kuifunika Iokote.

Kwasasa ana ngoma yake mpya inayoitwa Niteke na inafanya vizuri, ambapo imeshatazamwa zaidi ya mara laki moja katika mtandao wa YouTube.