
Awali kesi iliyokuwa inatakiwa kusikilizwa ni ya kuomba dhamana iliyowasilishwa juma lililopita mahakamani hapo na mawakili wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).
Kwa mujibu wa sheria makosa aliyosomewa Erick Kabendera hayana dhamana na hivyo karudishwa rumande kwa ajili ya kuendelea kusikiliza dhamana, na mshatakiwa baada ya kusomewa mashtaka hayo hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hiyo, na kesi hiyo imeahirisha hadi Agosti 19, 2019.
Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, Faraja Nchimbi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon walimsomea Mshtakiwa mashtaka matatu ambapo katika shtaka la kwanza mshatakiwa inadaiwa kati ya Januari mwaka 2015 na Julai 2019, maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kabendera na wengine ambao hawapo mahakamani walitoa msaada kwenye genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha.
Katika shitaka la tatu, Kabendera anadaiwa kati ya Januari, 2015 na Julai 2019 maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam bila sababu za msingi alikwepa kulipa kodi Sh 173,247,047.02 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Aidha, katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha, inadaiwa katika tarehe hizo mshtakiwa alitakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zimetokana na zao la kusaidia genge la uhalifu na kukwepa kodi.