Haji Manara.
Haji alionesha kuchukizwa na moja ya mashabiki kumtolea matusi mtandaoni huku akimhusisha hadi mama yake mzazi ambapo alidai kuwa kitendo kile ni 'upumbavu' na haikumaanisha kuwa mashabiki wote wako vile na atakayeonesha video ikionesha akisema maneno yale atatoa kiasi cha shilingi milioni tano.
Kupitia ukurasa wake wa 'Instagram' ameandika kuwa, "Sikuwa hata nataka kuliibua tena hili ila watu wangu wa karibu wamenishauri nijibu sababu uongo ukizungumzwa sana unaaminika ni kweli mimi siwezi na sijawaita mashabiki wa Simba ni wapumbavu, nimetaja neno pumbavu kwa mtu aliyenitukania mama yangu matusi mazito yasioandikika".
"Msilishwe matango pori na watu wenye chuki na hasadi, ninatoa Milioni tano kwa mtu yoyote atakaeisambaza 'clip' inayoonyesha mimi nimesemema mashabiki wa Simba wapumbavu", ameongeza Haji Manara.