Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania Dkt Seif Rashid.
Waziri wa Afya wa na ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wamepatikana raia wawili wa kigeni wenye dalili za kuugua ugonjwa huo ambao walikimbizwa katika kituo maalum cha uchunguzi wa ugonjwa wa Ebola wilayani Temeke.
Wagonjwa waliohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo awali ni wa kutoka Benin na Mtanzania mmoja lakini baada ya kuchunguzwa vipimo vimeonesha hawana maambukizi ya ugonjwa huo.
Nchi kadhaa za Afrika zimeanza kuchukua tahadhari kutokana na kusambaa haraka kwa ugonjwa huo hatari ambao mpaka sasa umeshaua watu 1068.
Ugonjwa wa ebola uliibuka Februari mwaka huu huko nchini Benin na kusambaa haraka hadi katika nchi za Liberia, Sierra Leon na Nigeria ambapo Shirika la Afya Ulimwenguni limeutaja ugonjwa huo kama janga la kimataifa.