Mkuu wa kitengo cha 'Customer care' akitoa maelekezo kwa washiriki wa Dance 100% kabla hawajaanza ziara ya kuangalia utendaji kazi wa kitengo hicho
Katika ziara hii, wasakata dansi hawa mahiri wamepata nafasi ya kutembelea vitengo mbalimbali vya kampuni hii na kuweza kujifunza namna inavyoendesha kazi zake.
Kuhusiana na ziara hii, mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw. Kelvin Twissa amepata nafasi ya kuzungumza na vijana hawa na kuwahamasisha kujitahidi ili kuweza kugeuza vipaji vyao kuwa biashara, na pia kutumia huduma ya mawasiliano ya Vodacom kujitangaza na kuionyesha dunia uwezo wao, na pia kujijengea imani kwa wadau wanaoweza kuvutiwa kufanya kazi pamoja nao.
Bw. Kelvin ameongeza kuwa, udhamini wao kwa mashindano haya ni kutokana na kukua kwa muziki kama ajira Tanzania, nafasi ambayo inawawezesha vijana kukutana, kufanya kazi pamoja na pia kuleta burudani kwa jamii.
Kwa upande mwingine, muwakilishi kutoka EATV, Bi Happy Shame amewataka washiriki hawa kutumia vizuri nafasi waliyopatiwa na EATV kwa kushirikiana na Vodacom kwa nidhamu na kujituma.
Kivutio kikubwa katika mashindano haya ni pale washiriki walipopata nafasi ya kuonesha na kuwafundisha maafisa kutoka Vodacom mitindo mbalimbalu ya kudansi.
Mashindano haya kwa mwaka huu yanakwenda kwa swaga #2014Dance100%