
Sister P kushoto na Flaviana Matata kulia
Sister P ameiambia eNewz sababu ya kubadilisha jina hilo ni kutokana na watu wanavyomuita kuwa ni mtu mwenye Matata pamoja na uwezo mkubwa wa kufanya vitu tofauti kama kuimba.
'Mimi nilikuwa napita mtaani nikasikia shabiki ananiita oyaa sister P mbona kimya fanya uachie ngoma si unajua wewe ni mtu poa sana yaani hauna matata kabisa basi waliokuwa pembeni kuanzia siku hiyo wakaanza kuniita P Matata na mimi sikuona tabu nikaona freshi tu acha liwe jina langu" amesema mkali huyo.
Hata hivyo Sister P anasema hajui kama Matata jina lao la ukoo 'Grace au Flaviana' lakini yeye kwa upande wake analitumia kama a.k.a tu kutokana na mambo yake anayoyafanya na jinsi anavyoishi na watu wake mtaani mashabiki zake kwa ujumla.