Gambo ametoa kauli hiyo leo, Juni 15 mara baada ya ibada ya sikukuu ya Eid iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo mkoani Arusha na kuwataka Bakwata kukemea tabia hiyo.
Mh. Gambo amesema kwamba tabia ya baadhi ya misikiti kufundisha waumini wake mchezo wa kareti ndani ya misikiti haifai na inapaswa kukemewa.
“Baadhi ya misikiti kufundisha karate haifai naomba niwapongeze Bakwata kwa kukemea tabia hii na ninawaomba muendelee kulisimamia hili” amesema Gambo