Tuesday , 12th Jun , 2018

Katibu Mkuu wa shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini (TBF) Michael Mwita amesema kuwa asilimia themanini ya Kikosi cha Mpira wa kikapu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 ni zao la Sprite Bball Kings 2017.

Mwita amesema hayo wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo mwaka 2018 ambapo amesema kuwa matunda ya Sprite Bball Kings yameonekana hivyo yanatakiwa kuungwa mkono na kuthaminiwa katika sekta ya michezo.

“Asilimia themanini ya wachezaji wanaounda timu ya kikapu ya taifa ni zao la Sprite Bball Kings kwani vijana wale baadaya kushiriki michuano ile walipata mwanga ni wapi wataendeleza vipaji vyao vilivyoibuliwa ndipo shirikisho tulichagua hapa hapa kupitia fainali zile za mwaka jana”, amesema Mwita

Lengo la mashindano ya Sprite Bball Kings ni kuibua vipaji na kuutangaza mchezo huo nchini ambapo mshindi wa kwanza atajishindia zawadi ya shilingi Millioni kumi. Usahili wa timu shiriki, utafanyika kwa siku moja ya Jumamosi Juni 16, katika viwanja vya Mlimani City Mall kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.