Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) Dkt Hellen Kijo-Bisimba.
Hatua hiyo iwapo itatekelezwa, itakuwa na athari kubwa kwa zaidi ya Watanzania 18,000 ambao baadhi yao kituo hicho imefungua mashauri ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika mahakama mbalimbali nchini na ambayo yanaendelea katika mahakama hizo.
Akizungumza katika mahojiano na East Africa Radio jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho Dkt Helen Kijjo—Bisimba, ameitafsiri tozo hiyo kama njama za chini chini za kutaka kukifuta kituo hicho, kwani mazingira ya namna ilivyopata baraka na kusajiliwa na mahakama yanatia shaka kwa madai ya LHRC kutoshirikishwa.
Aidha, tofauti na inavyodhaniwa na wengi kwamba kituo hicho kimekuwa kikipingana na serikali; Dkt Bisimba amesema LHRC imekuwa msaada kwa jamii na hata kwa serikali yenyewe na kutolea mfano namna wanasheria wa kituo hicho, walivyochangia ushindi wa serikali katika kesi baina yake na iliyokuwa kampuni ya kusambaza maji jijini Dar es Salaam ya Bywater, kesi iliyofunguliwa katika mahakama ya kimataifa ya migogoro ya kibishara.
Kwa mujibu wa Dkt Bisimba, hata kesi ya Dowans serikali ingeweza kushinda na kuepuka kulipa kiasi kikubwa cha pesa iwapo ingewashirikisha wanasheria kutoka asasi za kiraia ikiwemo kituo cha sheria na haki za binadamu na kwamba hatua yao ya kupinga malipo ya Dowans ilikuwa na nia njema ambayo ingeungwa mkono na serikali.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa jumla ya mashirika matatu pamoja na mwandishi wa habari mmoja ndio waliofungua kesi kupinga hukumu ya kesi ya Dowans kusajiliwa katika mahakama kuu nchini lakini