
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi huo kupitia ukurasa wao maalum wa Klabu na kusema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukuza ufanisi pamoja na morali kwa wachezaji wake.
"Simba Sports Club imekuwa mbele katika kuanzisha vitu vipya. Ikumbukwe kuwa Simba Sc ndio ilikuwa ya kwanza kuwa na tunzo za wachezaji wake kila mechi na kila mwezi. Mo Simba Award zimeanzishwa na Mwekezaji katika klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji kwa lengo la kutoa zawadi kwa wanafamilia wa Simba ambao wamesaidia klabu kupata mafanikio kwa msimu wa 2017/2018", imesema taarifa hiyo.
Aidha, Tuzo hizo za Simba ambazo zinaitwaa 'Mo Simba Award' zinatarajiwa kuwa na vipengele 17 ambavyo vitahusisha wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, mashabiki na wasimamizi wa mchakato wa mabadiliko.
Kwa upande mwingine, taarifa hiyo imesema sherehe za kuwakabidhi zawadi washindi zinatarajiwa mwezi huu wa Juni licha ya tarehe husika kutojazwa kwa sasa.