Thursday , 3rd Jul , 2014

Timu shiriki za michuano ya ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania (RBA) zimetakiwa kukamilisha malipo kabla ya Julai 31 ili ziweze kushiriki michuano hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa Timu za Mkoa wa Dar es salaam wakichuana katika moja ya mchezo wa Ligi ya Mkoa Msimu Uliopita

Timu shiriki za michuano ya ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania (RBA) zimetakiwa kukamilisha malipo kabla ya Julai 31 ili ziweze kushiriki michuano hiyo.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa RBA Jimmy Nkongo amesema kwa kawaida wanatarajia kuwa na timu 16 lakini kabla ya kushiriki zinatakiwa kukamilisha malipo ya timu zao yakiwemo ada za Mwaka, Ada za Usajili na Ada za Ushiriki.

Nkongo amesema hadi kufikia muda huo uliopangwa kama kuna timu itakuwa haijakamilisha malipo hayo kwa mujibu wa sheria za Chama timu hiyo itakuwa imejitoa katika ushiriki wa michuano hiyo kwa mwaka huu.

Tags: