Saturday , 28th Jun , 2014

Jamii ya Watanzania wenye uwezo kiuchumi wametakiwa kutumia sehemu ya uwezo wao kushiriki na watoto yatima na wenye uhitaji ili kujenga jamii yenye kuonesha upendo kwa wenye mazingira magumu.

Baadhi ya watoto wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha Kimbangulile.

Jamii ya Watanzania wenye uwezo kiuchumi wametakiwa kutumia sehemu ya uwezo wao kushiriki na watoto yatima na wenye uhitaji ili kujenga jamii yenye kuonesha upendo kwa wenye mazingira magumu.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Jumuiya ya Enaboishu wakati waliposhiriki chakula cha mchana na kutoa kingine kitakachotumika katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kutoa chakula hicho leo, Katibu wa Enaboishu, Godfrey Severe amesema msaada pekee kwa watoto yatima ni kuonesha upendo kwa kuwa karibu nao na kuwapa kidogo walichonacho kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa.