Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii - ESRF Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na katibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Jumanne Sagini wakati wizara hiyo kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) pamoja na Taasisi utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), ikitoa muelekeo kuhusu mwenendo wa kufikia malengo ya milenia ya mwaka 2015
Kwa upande wake Afisa wa UNDP Amon Manyama amesema kasi ya utekelezaji wa malengo ya Milenia ya 2015 hairidhishi kutokana na serikali kutekeleza pasipo kuzingatia rasilimali zilizopo nchini.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, ESRF Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo amesema malengo hayo yamewekwa pasipo kuzingatia mgawanyo sahihi wa vipaumbele katika sekta ya elimu na umechangia kutofikiwa kwa malengo hayo.