
Lissu ameyasema hayo leo mchana wakati akifanya mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya Kijerumani (DW).
"Madaktari wangu wamenihakikishia kuwa nitarejea nchini na nitaendelea na shughuli zangu kama kawaida", amesema
Katika hatua nyingine Lissu amesema anachokumbuka katika tukio hilo wakati wanaingia getini kulikuwa na gari moja nyeupe limesimama huku kulikuwa na watu wawili.
"Walikuwa watu wawili, mmoja mwembamba niliona akishuka huku ameshika "Machine gun" baadaye najishtukia nipo hospitali Nairobi", ameongeza.
"Ninachoshangaa ndani ya ile nyumba kuna ulinzi mkali walikuwa wapi walinzi wakati nashambuliwa", amesema.