
Rais Magufuli ametangaza msamaha huo leo mjini Dodoma kwenye sherehe za Uhuru wa miaka 56 ya Tanganyika, ambapo pia ametoa msamaha kwa wafungwa 8,157.
“Nimeamua kusamehe wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha huu, 1828 watatoka leo, 6329 wamepunguziwa muda wa kukaa gerezani”, amesema Rais Magufuli.
Baada ya kutangaza hivyo rais Magufuli akaongeza kuwa katika msahama huu nimeamua kuisamehe familia ya Nguza Viking na kuanzia sasa wawe huru kulingana na taratibu za kimagereza.
"Na kwa mujibu wa ibara hiyo hiyo ya 45, nimeamua kusamehe familia ya Nguza Viking au Babu Seya na ndugu Johnson Nguza au Papii Nguza waaachiwe huru kuanzia leo", amesikika Rais Magufuli akisema mbele ya halaiki ya watu ambao walifika kuhudhuria sherehe hizo katika viwanja vya Jamhuri.
Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12 mwaka 2003 na walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003, wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10, na Juni 25, 2004 Mahakama iliwatia hatiani na kuwahukumu kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.