Friday , 8th Dec , 2017

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) kuchagua kiongozi ambaye atakuwa anajali wanawake na siyo kujali tumbo lake.

Dkt. Magufuli ametoa wito huo leo wakati akifungua mkutano wa wajumbe wa CWT Mkoani Dodoma wambapo amesema watakapokuwa wanachagua viongozi wasiangalie wamepewa kanga kiasi gani, wala wamelipiwa hoteli ya aina gani.

Nataka mchague kiongozi wa kujali wanawake na sio kujali tumbo lake na awe mtetezi na shida zao wala habagui, Walaa msimuangalie anayesema anadhaminiwa na nani” amesema Rais Dkt. Magufuli.

Ameongeza “Chama tunakata kiwe cha wananchi na sio cha mtu binafsi na kiongozi atakayechaguliwa aendane na mabadiliko ya ndani ya chama,” amesema Rais Dkt. Magufuli.

Tukio hilo limeambana na tukio la aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira kuhamia CCM.