
"Umaarufu ni gharama, watoto wangu nawaacha wachague wenyewe kipi wanataka wafanye,wachague umaarufu wa maisha ya kawaida, ila kitu cha kwanza lazima tuwaelekeze katika elimu",amesema
Banana Zorro ni msanii ambaye hana mambo mengi katika maisha yake ya usanii, hachanganyi kati ya usanii na familia.
"Unapochanganya familia na usanii unaweza kuharibu mfumo mzima wafamilia , usichanganye vitu hivi". Banana amesema.
Banana Zoro ambaye amezaliwa katika familia ya muziki,amewahi kutamba na ngoma kali kama vile Mama yangu,Nzela aliyoimba na bendi yake ya B-band na Mapenzi gani.