Licha ya watu wengi kumtaka Ostaz kumuomba PNC na wasanii msamaha hadharani kwa kitendo chake cha kusambaza tukio la PNC kumpigia magoti kumuomba msamaha, Msanii huyu ametueleza kuwa haoni ajabu na anawashangaa wote waliokerwa na ishu hii ambayo yeye anaichukulia poa tu.
Tayari lebo ya Mtanashati ina rekodi za kufanya matukio kadhaa kwa lengo la kuleta chachu ya umaarufu wake, na tukio hili tata linahesabiwa kama moja ya jaribio la kusaka umaarufu la Ostaz.
PNC pamoja Ostaz kwa pamoja wanatarajia kutoka na ngoma ambayo inakwenda kwa jina Thamani Yangu ambayo imefanya na mtayarishaji muziki Mazuu ikiashiria kurejea kwa PNC chini ya lebo ya Mtanashati.