Tuesday , 27th May , 2014

Klabu ya Bongo Movie, kwa mara nyingine imepata pigo la kuondokewa na moja ya wasanii wake, Rachel Haule aliyefariki dunia usiku wa jana baada ya kupata tatizo wakati akijifungua.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bongo Movie Klabu, Steve Nyerere, siku ya leo wasanii walikutana pale Leaders Club kwa ajili ya kujipanga kwa msiba ambapo habari kutoka kwa shemeji wa marehemu Issa Ahmad amesema msiba upo nyumbani kwa mjomba wake Sinza Palestina.

Marehemu amepoteza maisha yeye pamoja na mtoto aliyekuwa akijifungua, na eNewz inawatakiwa mapumziko mema mahala pema peponi pamoja na faraja kwa wafiwa na tasnia ya sanaa ya filamu kwa ujumla.