Msanii wa filamu nchini Jacob Stephen
Hayo yameibuka baada ya kelele nyingi katika mitandao ya kijamii ikiwasema waigizaji pamoja na watayarishaji wa filamu nchini kukosa ubunifu wa kutosha na sasa kushinikiza serikali izuie kuingiza filamu zinazotoka nje ya nchi.
“Kwenye shida mimi sitajali nani ananisaidia ili mradi anagusa maslahi yangu, ugali wangu. Nakiri sinema zetu zina mapungufu mengi lakini hilo siyo sababu za kuacha kudai haki zetu, ni kama mgonjwa akiumwa leo anapelekwa kwa mganga kesho anapelekwa kuombewa, anatetea roho yake”. Ameandika Jb kupitia mtandao wake wa kijamii instagram
Vilevile JB, amesema hakuna aliyesema filamu za nje zifungiwe ila wanachotaka ni zifuate utaratibu kama wanavyofuata wao wenyewe.
“Ngoja tumalize hili tusichanganye na pia hakuna aliyesema zifungiwe hapana zifuate utaratibu kama sisi tunavyofuata hizo hizo ‘movie’ zetu mbovu ndiyo zinatuwezesha kuishi lakini pia lazima mfahamu biashara hii ni kubwa kuliko mnavyodhania, muvi mbili zinanitosha kuishi kwa mwaka mzima, ushawaza ni kiasi gani ?”. Alisisitizia JB
Kwa upande mwingine amewashukuru wananchi kwa kumpa ushirikiano katika kazi zake zaidi ya 50 kwa miaka 20 tangu anze fani hiyo.