Kocha huyo ametamka kuwa atatangaza hadharani hatma yake mwezi April kabla ya msimu huu kumalizika, huku akikiri kuwa kwa sasa mashabiki wa timu hiyo hawana furaha kutokana na uwepo wake, hali iliyosababisha baadhi yao kufanya maandamano baada ya kipigo cha mabao 5-1 ilichokipata juzi kutoka kwa Bayern Munich.
Amesema anaheshimu maoni ya mashabiki wa timu hiyo walioandamana, huku akisema kuwa katika miaka yake 20 aliyoitumikia klabu hiyo amekuwa akijitahidi kuwafanya mashabiki wawe na furaha, lakini timu inapofanya vibaya anagundua kuwa mashabiki hao hawana furaha.
"Nimefanya kazi kwa miaka 20 kuwafanya wawe na furaha, mambo yakiwa hivi nagudua kuwa hawana furaha, siwezi kuwahukumu kwa hilo ilimradi mimi ninaendelea na kazi zangu za kila siku kwa moyo wote". Wenger amewaeleza waandishi wa habari kuelekea mchezo wa robo fainali kombe la FA Jumamaosi hii dhidi ya Lincoln

Mashabiki wakiandamana, juzi usiku
Ameongeza kuwa anafanya kazi hiyo akiwa amebeba taswira ya klabu na siyo taswira yake, hivyo jinsi wanavyomuona kwa sasa, kama kuna tatizo basi tatizo hilo haliko upande wake.
“Tangu nimekuja hapa, nimethibitisha na nimedhihirisha kuwa nina mapenzi ya dhati na pia ni mwamonifu kwa klabu hii, nafikiri nimefanya maamuzi sahihi na nitaendelea kuheshimu desturi za klabu hii” Amesema Wenger
Pia kocha huyo amekanusha taarifa za kuwa tayari amekwishawaaga wachezaji wake, na kusema kuwa taarifa hizo ni za kupuuza.
Kwa upande mwingine, Wenger ameendelea kupinga kadi nyekundu ambayo mchezaji wake Laurant Kosccielny kuwa haikuwa halali na kwamba hiyo ndiyo sababu ya kufungwa kwa kuwa wao walikuwa bora zaidi ya Bayern akama ingekuwa ni wachezaji 11 kila upande





