Monday , 19th May , 2014

Mrembo aliyewahi kushikilia taji la Miss Universe Kenya, Rachel Marete amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, taarifa zinazosambazwa juu yake kuwa na asili ya Tanzania si za kweli na hajawahi kusema kitu kama hicho.

Rachel Mrete

Rachel ambaye anapendelea kuweka maswala ya familia yake mbali na vyombo vya habari, amesema kuwa, ameguswa sana kuona maelezo kuhusiana na marehemu baba yake kuwa alikuwa ni mwanasiasa mahiri wa Tanzania, kitu ambacho hakusema yeye.

Rachel ambaye pia anafanya kazi zake za muziki, safari hii ameachia video ya kazi yake mpya ambayo inakwenda kwa jina Nguvu.