Saturday , 26th Nov , 2016

Tume ya uchaguzi katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani limepokea ombi la kurudiwa kuhesabu kura za uchaguzi uliopita ambapo mshindi alikuwa Donald Trump aliyeshinda kwa kura chache wiki mbili zilizopita.

Jill Stein - Aliyekuwa mgombea urais Marekani

 

Ombi la kurudiwa kuhesabu kura liliwasilishwa na mgombea wa urais kupitia chama cha  Green Party Jill Stein ambaye pia ametaka kura zirudiwe kuhesabiwa katika majimbo ya  Michigan na Pennsylvania.

Hata hivyo ikiwa Hillary Clinton atashinda jimbo hilo hakutabadilisha matokeo ya ushindi wa Trump kwani lina kura 10 pekee za wajumbe wa uchaguzi.

 Kamisheni hiyo imethibitisha kupokea maombi hayo na kuainisha kutoa maelekezo muda si mrefu.