
Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro na kiongozi wa Mapinduzi ya Kikomonisti amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.
Mdogo wake ambaye ni rais wa Cuba kwa sasa Raul Castro amesema kuwa amiri jeshi mkuu huyo wa mapinduzi ya Cuba amefariki dunia jana usiku.
Fidel Castro aliiongoza Cuba chini ya serikali ya chama kimoja kwa karibu miaka 50, kabla ya mdogo wake Raul kutwaa madaraka mwaka 2008.
Kifo cha Castro kimetokea ikiwa ni miezi michache tu kupita tangu kiongozi huyo wa mapinduzi ya Kikomonisti kujitabiria kuwa kifo chake kipo karibu.