Thursday , 24th Nov , 2016

Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji maalum kwa kutumia darubini kuhamisha misuli na mishipa ya damu toka kwenye mguu kwenda sehemu nyingine chini ya mguu.

Madaktari bingwa wakiendelea na upasuaji.

 

Daktari Bingwa wa upasuji ambaye ni Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Ibrahimu Mkoma ambaye ameshiriki katika upasuaji huo amesema upasuaji huo wa aina yake ambao ni wa mara ya kwanza kufanyika nchini ukisimamiwa na madaktari bingwa zaidi ya wanne kutoka Tanzania na Austraria.

Upasuaji huo kwa mara nyingi hufanyika kwa muda wa saa sita mpaka saba, ambapo kwa mujibu wa Dkt. Mkoma unagharamu kiasi cha dola elfu 40,000 ikiwa ni gharama ya upasuaji pekee.

Dkt. Mkoma ameongeza kuwa wana mpango wa kuanzisha chuo maalum kwa ajili ya upasuaji huo nchini ili kuhakikisha wanapata wataalamu wengi zaidi na wanawafikia wagonjwa wengi hasa wale wa maeneo yasiyofikika kwa haraka.