
Rais wa Zambia, Edgar Lungu
Dkt. Mahiga amesema wakati wa ziara hiyo, Rais Lungu atasaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania.
Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na ushirikiano wa masuala ya anga, ulinzi na usalama, ushirikiano katika masuala ya uhamiaji, na kuweka utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Akiwa nchini Rais Lungu pia atatembelea Bandari ya Dar es Salaam, reli ya Tazara, na bomba la mafuta la Tazama.
Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya Afrika Balozi Samweli Shelukindo amesema utekelezaji wa mikataba hiyo utaleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.