Meneja wa Idara ya Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa Bw. Daniel Masolwa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema dhumuni la kuadhimisha siku hiyo ni kuongeza uelewa mpana kwa watumiaji wote wa Takwimu Afrika kuhusu umuhimu wa takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo katika sekta zote za kijamii na kiuchumi.
Bw. Masolwa ameeleza kuwa kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Kuimarisha Takwimu za Kiuchumi kwa Mtangamano wa Kikanda, Mabadiliko ya Miundo na Maendeleo Endelevu".
Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika hufanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba ambapo huandaliwa na kaulimbiu mbalimbali zinazohusiana na umuhimu wa takwimu katika kupanga maendeleo na kutunga sera katika Bara la Afrika.