Tuesday , 1st Nov , 2016

Idadi ya mauzo katika soko la hisa la Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 39 kutoka shilingi bilioni 3.8 na kufikia shilingi bilioni 5.3 kwa mujibu wa taarifa za mwenendo wa biashara katika soko hilo katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Patrick Mususa

 

Meneja Miradi na Biashara wa soko hilo Bw. Patrick Mususa amesema katika kipindi hicho, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 91 kutoka hisa milioni tisa na laki nane hadi hisa laki nane na elfu sitini na tisa.

Aidha, Mususa amesema ukubwa wa mtaji wa soko nao umepanda kwa asilimia, kutoka shilingi 21.6 hadi shilingi trilioni 21.8, huku ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani ukiwa umepanda kwa asilimia 0.4 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa wiki iliyopita.