Thursday , 8th May , 2014

Kocha mkuu wa timu ya Dar es salaam Young Africans Mholanzi Hans Van Der Pluijm, ameondoka rasmi katika timu hiyo na kurejea kwao.

Aliyekuwa kocha wa Yanga hans Van Der Pluijm

Kocha mkuu wa timu ya Dar es salaam Young Africans Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye uongozi wa Yanga uliingia naye mkataba wa muda mfupi wa miezi 6 ambao unamalizika mwezi June ameondoka rasmi katika timu hiyo na kurejea kwao.

Van Pluijm ambaye inasemekana alikua na mkataba na timu moja huko Saud Arabia amesema kuwa hatosaini mkataba na Yanga kwakua amepata mkataba mnono kutoka nchini Saud Arabia

Kwa upande wa Uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu wa timu hiyo Beno Njovu amesema kuwa kuondoka kwa kocha huyo si tatizo kwani wana muda wa kutosha kutafuta kocha mwingine ambaye atabeba jukumu hilo.

Njovu amesema kocha Pluijm aliwapa taarifa hiyo mapema kupitia kamati ya utendaji na amewaahidi kuwasaidia kutafuta kocha bora atakayechukua timu hiyo kwaajili ya msimu ujao na hivyo anawatoa shaka mashabiki kwani walishaianza mapema kazi ya kutafuta kocha mwingine.