Tuesday , 20th Sep , 2016

Kundi la D.D.I Crew ambalo linashiriki fainali za Dance100% 2016 ambazo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam limesema kuwa kundi hilo ni dogo kiumri ila ni wakubwa kiakili.

Dundi la DDI Crew wakiwa na Mtangazaji Zembwela baada ya kipindi cha SUPAMIX cha EA Radio

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kundi hilo Samson Shobigo akiwa katika kipindi cha SupaMix kinachorushwa na East Africa Radio na kusema kuwa kundi hilo limejipanga vizuri katika kunyakua kitita cha milioni 7 na tayari wana mikakati ya kutumia fedha hizo katika miradi ya maendeleo.

“Sisi tumejipanga vyema katika kushiriki fainali Jumamosi na sisi ni wazoefu katika mashindano ya kucheza, tumeshakwenda hadi nje ya nchi kwa ajili ya shughuli ya dansi, hivyo watu wakae mkao wa kushuhudia mambo mazuri sana kutoka kwetu” Amesema Shobigo.

Kwa upande wake binti pekee anayeshiriki Shindano la Dance100% maarufu kwa jina la Kibibi amewataka kinadada kutoogopa kutumia fursa zinapojitokeza kwani kupitia Dance100% inamfanya atambulike kwa kipaji alichonacho ndani ya jamii.

Shindano la Dance100% linaendeshwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom na Coca- Cola na kuoneshwa na EATV kila Jumapili saa moja jioni.

Tags: