Kikosi cha Mbeya City
Kocha mkuu wa timu ngumu ya Mbeya City ya jijini Mbeya mzalendo Juma Mwambusi amewataka wachezaji wa vilabu chipukizi ambao ndio kwanza wamepata nafasi ya kuonekana kwa mara ya kwanza katika ligi kuu ya Tanzania bara kuwa watulivu katika kipindi hiki cha usajili kwakuwa maamuzi yoyote ya papara yatakua ni majuto kwa vipaji vyao na maisha yao ya kisoka kwa ujumla
Mwambusi amesema hayo mara baada ya kuwepo na tetesi za baadhi ya nyota wa timu ya Mbeya City kuwaniwa na vilabu vikubwa vya Simba, Yanga na Azam,
Aidha Mwambusi amesema si kwamba anataka kuwazuia wachezaji wake wasijiunge na timu nyingine bali anaangalia mustakabali wao wa maisha ya kisoka ya baadae.