Eneo lililokuwa na nyumba za Kota Magomeni, linavyoonekana baada ya nyumba hizo kubomolewa ili kupisha shughuli za mradi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amesema kuwa Rais Magufuli ameamua kuwa waliokuwa wapangaji katika nyumba za serikali za 'Magomeni Kota' Dar es Salaam, wauziwe nyumba 644 zitakazojengwa na serikali.
Waziri Lukuvi amesema Rais pia ameamua kuwa umiliki wa nyumba kama hizo katika mikoa 20 nchini, uhamishiwe serikali kuu badala ya kuwa chini ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI.
Wakazi hao wapatao 610 waliokuwa wapangaji katika kota za Magomeni waliingia mkataba Januari, 2011 wa kukubaliana na Manispaa ya Kinondoni kulipwa shilingi elfu tisini kwa mwezi kama gharama za upangaji ili wakazi hao kupisha ujenzi wa mradi wa uwekezaji kwenye eneo ambalo nyumba walizokuwa wamepanga zilikuwepo na baadae wapewe kipaumbele katika mradi huo.
Mkataba huo ulidaiwa kuwa ni miongoni mwa mikataba mibovu na Serikali inachukua hatua za kubadili usimamizi wa nyumba hizo kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ili kuusimamia mkataba wa ujenzi wa Nyumba hizo.
Lukuvi anasema kufuatia nyumba hizo kushindwa kuendelezwa na Halmashauri kama ilivyokuwa lengo la serikali kuu kuzipa mamlaka Halmashauri sasa nyumba hizo zitakuwa chini ya serikali kuu ili wanufaika wakuu wawe wapangaji walioondolewa kwa kuuziwa nyumba hizo.
Wakazi hao wa nyumba kongwe zilizokuwa Magomeni kota waliingia makubaliano na Halmashauri kabla ya kuondoka kwenye eneo hilo januri 2011, eneo lenye ukubwa wa ekari 34.
Uamuzi huo unawanufaisha wapangaji wengine waliopo katika mikoa 20 ya Tanzania ambao wamekuwa wakiishi katika kota hizo kongwe za serikali






.jpeg?itok=uqe_Ivr6)