Wakulima wakiwa wanahifadhi mahindi yao katika mifuko kwa ajili ya Mauzo
Hayo yamebainishwa na afisa Kilimo wa Mkoa huo Grace Macha na kusema hatua hiyo inakuja kufuatia malalamiko kutoka kwa wanunuzi na watafiti wa mazao waliothibitisha baadhi ya wakulima kutokujua matumizi ya viautilifu hivyo.
Afisa Kilimo huyo amesema kuwa bado kuna haja ya maafisa ugani wa mkoa huo kuendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuachana na utaraibu wa kuhifadhi mazao kwa kutumia viatilifu ili kuepusha madhara zaidi ya mazao na afya za walaji.
Kwa upande wake mshauri mwelekezi kutoka Marekani Benadeta Magedele, ambacho kimefanya utafiti wa mifuko ya kutunza mazao kwa njia ya asili bila kuweka dawa amesema utaratibu huo uko salama kwa mazao kukaa kwa muda mrefu na kuendelea kuwa salama kwa walaji.