
LINEX SUNDAY MJEDAA
Hata hivyo Linex anadaiwa kuwa na mahusiano na mwanamke wa kizungu na Enews ilitaka kujua kama bado anaendelea na mmarekani huyo na nini malengo yake kwa sasa, ambapo Linex alisema hajawahi kuachana na mpenzi wake huyo wa kizungu.
Linex pia amesema sababu za yeye kutoenda kuishi na mzungu wake Marekani ambapo amedai kwamba sababu kubwa ni kuhofia kupoteza soko lake la kimuziki hapa nchini huku akisisitiza kwamba alitumia nguvu nyingi sana kutangaza muziki wake hapa bongo, hivyo hataki kupoteza heshima yake ya muziki na kwamba mpezi wake huyo huja mara kwa mara nchini.
Baadhi ya watu wamekuwa wakimdisi sana Linex juu ya suti zake ambazo amekuwa akizivaa katika video zake na kusema kuwa suti hizo huwa zinamvaa na hapendezi.
Swali lilikuwa ni vipi kuhusiana na wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa na Belle 9, atavaa tena suti au ataachana nazo? Endlea kufuatilia Enewz