Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala
Hayo yamebainihwa katika kikao cha Arobaini na Saba cha mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja linaloendelea mjini Dodoma, katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala akijibu swali la Mbunge wa Chemba Juma Nkamia aliyetaka kujua mpango wa serikali kudhibiti upandaji holela wa dawa nchini.
Akijibu Swali hilo, Mhe. Hamis Kigwangala amesema asilimia 80 ya dawa hupanda bei kutokana na mabadiliko ya sarafu ya dunia hivyo serikali imepanga kuongeza kiwango za uzalishaji nchini pamoja na kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa dawa.
Mbunge wa Mkuranga, Mhe.Abdallah Ulega ameitaka serikali kuangazia mazinmgira duni ya wafanyakazi wa viwandani ili kuondokana na ujira mdogo wanaoupata.
Kwa upande mwingne, Mhe. Nkamia ameomba muongozo kwa Naibu Spika baada ya mshtakiwa wa kumkashifu Rais kupitia mtandao wa kijamii, kuachiwa baada ya kulipia nusu ya fedha ya adhabu aliyotakiwa kulipa.