
Mshambuliaji matata wa klabu ya Leicester City na timu ya Taifa ya Uingereza Jamie Vardy (pichani).
Vardy alifunga goli la kusawazisha wakati Uingereza ikiitandika Wales magoli 2-1 amekua akipigiwa chapuo na baadhi ya wachezaji na wachambuzi wa michezo ambao wamemtaka kocha Roy Hogson kumpa nafasi ya kuanza ili aifungie mabao timu yake ya Taifa.
Nyota huyo ambaye anawaniwa na Arsenal ameshaifungia Uingereza mabao manne katika mechi tano zilizopita, ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali kufuatia mchango wake katika ligi kuu ya England akiifungia Leicester City magoli 24.
Endapo Uingereza itashinda itaungana na Ufaransa,Italia,Hispania na Uswizi ambazo tayari zimevuka hatua ya makundi baada ya kufanya vyema katika mechi zao.
Mpaka hivi sasa Uingereza inaongoza kundi lake ikiwa na alama nne katika mechi mbili ilizocheza ikifuatiwa na Wales wenye alama tatu huku Slovakia ikikamata nafasi ya tatu nayo Urusi inaburuza mkia kwa alama yake moja iliyoipata dhidi ya Uingereza.