Saturday , 18th Jun , 2016

Kocha wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys Bakary Shime amesema, mchango wa watanzania katika kuwapa moyo utasaidia kuweza kuondoa dhana ya kushindwa kila wakati.

Shime amesema, Shirikisho la soka nchini TFF imeonyesha njia ya soka la vijana linapoanzia hivyo ni wajibu wa jamii kutoa sapoti kwa kila idara kuhakikisha inafanya vizuri.

Shime amesema, vijana pia wameonyesha kama wanaweza hivyo watahakikisha wanapambana kuweza kuopa nchi sifa na kuweza kurudisha heshima ya soka la vijana nchini.

Shime amesema, timu peke yake haiwezi kufanya vizuri hivyo wanachohitaji kwa sasa ni sapoti ya kutosha kutoka kwa wananchi kwani kwa upande wa kikosi kimeshajiandaa kwa ajili ya mpambano.

Serengeti Boys na Shelisheli zitakutana June 25 mwaka huu jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza wa kuwania ushiriki wa Fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Madagascar.