Friday , 29th Apr , 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) imebakiza mechi zake 6 ambapo Simba SC watavaana na Azam FC jumapili hii katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, wakiwa na tofauti ya pointi moja ambapo Azam FC wako nafasi ya pili na Simba nafasi ya tatu.

Kesho Jumamosi Mabingwa Watetezi na Vinara wake Yanga wako huko CCM Kirumba kucheza na Toto Africans.

Kwa upande wa Yanga Kocha Mkuu, Hans van Pluijm, anayetoka Uholanzi, ameeleza kuwa watabadili staili kwa Mechi zao za Ugenini ukizingatia ubovu wa viwanja hivyo ili kushinda Mechi hizo.

Pia Kocha huyo alidokeza kuhusu kupigwa Benchi kwa Masta wake Donald Ngoma, Thaban Kamusoko na Vicent Bosou kwenye Mechi yao ya Juzi waliyocheza Uwanja wa Taifa na kuifunga Mgambo JKT 2-1. Pluijm alisema Wachezaji hao walihitaji kupumzika.

Hivi sasa Yanga iko kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa na Pointi 62 wakifuata Azam FC wenye 58 na Simba 57.

Hiyo Jumamosi huko Tanga Uwanja wa Mkwakwani, ipo mechi ya Mji huo kati ya African Sports na Coastal Union Timu ambazo zikifukuzana mkiani kwa Coastal kuwa ya mwisho kabisa ikiwa na Pointi 22 na juu yake ipo Sports yenye Pointi 23 huku zote zikiwa zimecheza Mechi 27 na kubakisha 3 tu.

Nako huko Mwadui Complex, Shinyanga, ipo mechi kati ya Mwadui FC na Stand United Timu ambazo zimefungana kwa Pointi, zikiwa na Pointi 34, huku Mwadui ikiwa imecheza Mechi 26 na Stand Mechi 25.

Jumamosi pia zipo Mechi nyingine mbili ambako huko Sokoine Mbeya, Tanzania Prisons itacheza na JKT Ruvu na huko Manungu, Morogoro ni Mtibwa Sugar na Mbeya City.

Jumapili ndio ipo Mechi tu ya kukata shoka kati ya Simba na Azam FC ambayo Azam FC wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 58 na Simba ni wa 3 wakiwa na Pointi 57 huku zote zikiwa zimecheza Mechi 25,