Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na na Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida
Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida, amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kukamilisha salama zoezi la upigaji kura katika uchaguzi Mkuu wa marudio visiwani humo.
Balozi huyo ameyasema hayo akizungumza mara baada ya kikao cha mafunzo, Osaka, ambacho kilishirikisha viongozi kutoka Halmashauri mbalimbali zilizokuwa nchini Japan kwa mafunzo ya kuwahudumia wananchi ili kuharakisha Maendeleo.
Balozi Yoshida amesema wananchi wa Zanzibar wameonesha ukomavu kwa kudumisha amani na utulivu wakati kwa uchaguzi huo ambao ulirudiwa baada ya kuafutwa kwa uchaguzi wa mwanzo wa Oktoba 25, mwaka jana.
Katika hatua nyingine Kalist Luanda ambae ni Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa amesema wamejifunza mengi kutokana na mafunzo kwa nchi ya Japani hivyo kupitia kauli mbiu ya hapa kazi wanaamini wataweza kuleta maendeleo ya haraka katika halmashauri zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Joseph Mkube amesema kuwa kwa mafunzo hasa kwenye sekta ya kilimo ataenda kuyatumia katika kukuza sekta ya kilimo katika halmshauri hiyo.