Tuesday , 23rd Feb , 2016

Msanii wa Bongo Fleva Nchini Peter Msechu amesema kati ya vyakula vyote, wali maharage ndiyo chakula anachokipenda zaidi.

Msechu ameyasema hayo alipokuwa anafanya mahojiano katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV na kuongeza kuwa chakula hicho humfanya hata akiwa kwenye gari akisikia harufu yake akili huvurugika kabisa.

Msanii huyo anaetamba na wimbo wake wa Nyota na Malava ameelezea pia suala la yeye kuwa mnene ni mwili wake ulivyo na hawezi kupungua na kuwa mwembamba kabisa hata siku moja.

Kuhusu msanii anayemvutia sana katika kazi zake Msechu amesema msanii Barnaba Classic ndiye anamvutia sana kwa namna anavyoandaa kazi zake pia aina yake ya maisha anayoishi.