Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame ambae pia ni Mwangalizi wa Uchaguzi nchini Uganda
Mwakilishi wa ofisi hiyo nchini Uganda Uchenna Emelonye amesema kitendo hicho cha kamisheni ya mawasiliano Uganda kinaingilia uhuru wa kujieleza akitaja mitandao husika kuwa ni pamoja na WhatsApp ambayo ilifungwa tangu saa mbili asubuhi.
Halikadhalika, mwakilishi huyo wa ofisi ya haki za binadamu Uganda amezungumzia kasoro zilizojitokeza wakati wa upigaji kura ikiwemo kuchelewa kwa vifaa vya kupiga kura au kutowasili kabisa akisema hilo linaengua baadhi ya wapiga kura.
Kwa upande wa mwangalizi wa uchaguzi huo kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Abdallah Makame ambaye ameongoza na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi amesema uchaguzi huo umekwenda vizuri licha ya kasoro zilizojitokeza.
Aidha Bw. Makame amesema kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo ambao umepangwa kuendelea tena leo baada ya baadhi ya vituo vingine kushindwa kupiga kura ingawa mpaka sasa amesema hawajashudia hujuma zozote za kuiba kura kutokana na mfumo uliopo.