Monday , 15th Feb , 2016

Nahodha wa Klabu ya Ngumi ya Ngome Suleiman Kidunda amesema, japo walipata changamoto katika mashindano ya taifa ya wazi ya mchezo wa ngumi lakini umoja wao kama timu umesaidia kuweza kushinda na kuwa Mabingwa katika mashindano hayo.

Kidunda amesema, hivi sasa wapo katika mazoezi kwaajili ya kuangalia mashindano yaliyo mbele yao ikiwa na pamoja na kusubiri kuitwa kambi ya Timu ya Taifa kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya kufuzu Olimpiki RIO mwaka huu.

Kidunda amesema, kila bondia katika kambi yao ya Ngome yupo tayari kw aajili ya kuweza kujiunga na timu ya Taifa kwa sababu bado wapo vizuri kwa ajili ya kuweza kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali.

Kidunda amesema, mazoezi ya muda mrefu ndiyo yalisaidia kuweza kupata ubingwa wa mashindano ya taifa ya wazi na kwa sasa makocha wanaendelea kujipanga ili kuweza kuendelea na ratiba nzima ya mazoezi ili kila Bondia aendelee kuuweka mwili wake sawa kwa ajili ya mshindano.