Mtandao wa Twita umesema kuwa umezisimamisha akaunti zaidi ya 125,000 tangu katikati ya mwaka 2015 kwa kutuhumiwa kutangaza matendo ya kigaidi.
Mtandao huo wenye makao yake makuu nchini Matrekani umesema akaunti zilizofungiwa zilikuwa na uhusiano na kundi linalojiita ISIS au dola ya kiislamu na kusisitiza katika taarifa hiyo kuwa kampuni hiyo inalaani matumizi ya Twitter kueneza ugaidi.
Mtandao wa Twita unawatumiaji milioni 500 duniani kote na taarifa hiyo imesema kwamba itashirikiana na mamlaka za kisheria juu ya matumizi mabaya ya mtandano huo na kuzitaka serikali zote duniani ikiwa ni pamoja na Marekani kuchukua hatua zaidi kudhibiti shuhguli za kimitandao.



