Naibu waziri wa Nchi Bunge Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde
Hayo yamesemwa leo Bunge na Naibu waziri wa Nchi Bunge Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde ambapo amesema wakala huwa utaweza kutimiza jukumu lake ipasavyo la kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri wa ndani na nje ya nchi.
Aidha Mhe Mavunde ameongeza kuwa mpango mwingine ni pamoja na kuandaa mkakati wa kukuza ujuzi nchini ambao utaanza kutekelezwa mwaka ujao wa fedha 2016/2017 ambao utajikita zaidi katika kuwezesha mafunzo ya vitendo mahali pa kazi.
Mhe. Mavunde alikuwa anajibu swali la mbunge wa Vwawa Mhe Japhet Ngailonga Asunga ambaye alitaka kujua mpango wa serikali katika kujua idadi ya wahitimu wa elimu waliokosa ajira na mpango wa kuwawezesha kupunguza tatizo la ajira kwa wanaomaliza elimu ya juu.