Haya yamebainishwa na wananchi waishio maeneo ya Mkwajuni na Jangwani jijini Dar es salaam wakati wakifanya mahojiano na kipindi cha Uswazi kinachorushwa na kituo cha EATV.
Wananchi hao wamesema kwamba vijana wengi hujisahau kwamba kuna maisha baada ya sikukuu na ndiyo maana hudiriki kutumia madawa ya kulevya kama bangi, kunywa pombe za viroba na hata kukaba watu kwa lengo la kujipatia fedha za chapchap.
Mmoja wa kijana aliyefahamika kwa jina moja la Silayo ameeleza kuwa vijana wengi wanakuwa wanaona kama maisha ni rahisi na wanaweza kufanya chochote msimu wa sikukuu jambo ambalo si sahihi hata kidogo na madhara yake ni makubwa.
Wakati huo huo wananchi hao wameelezea jinsi ambavyo wanavyoteseka sana katika kipindi cha mvua kutokana na serikali kutopanua kingo za mto wang'ombe ni chanzo kikubwa cha mafuriko katika eneo la Mkwajuni na Jangwani jijini Dar es salaam.
''Kama serikali ikifanya upanuzi wa mito ya Msimbazi na Wang'ombe ni hakika kwamba suala la mafuriko katika maeneo yetu itakua imekwisha maana mito hii hufurika sana na maji yanapozidi hubadilisha njia na kutudhuru sana ambapo maji huingia ndani na kufika hadi madirishani'' Alisema Bwn Alli mkazi wa Mkwajuni.
Ili kulinda maisha ya watu na mali zao hasa kipindi cha mvua Serikali iliamua kubomoa nyumba zote zinazozunguka maeneo oevu na mito na zoezi hilo lililofanyika eneo la jangwani liliacha mamia ya wananchi bila makazi ndipo waziri wa ardhi William Lukuvi alitoa agizo la kusitishwa kwa ubomoaji hadi Januari 05 2016 zoezi hilo litakapoanza tena nchi nzima kwa wakazi ambao wamejenga maeneo ya wazi, maeneo oevu, mabondeni na kando kando ya mito.