
Timu inaanza kuimarika, lakini haiwezi kuwa imara kwa kiwango cha juu kabisa ndani ya siku chache mpaka wapate muda ili kuendelea kufanya vizuri.
Kibaden amesema, Mchezo wa soka kila siku ni lazima kujifunza na wanaweza kuendelea kufanya vizuri, wakati mwingine wakaporomoka na kujifunza na kuendelea kwenda mbele.
JKT imeanza kuonyesha makali baada ya kuitandika Ndanda FC kwa mabo 3-1 Jumamosi ikiwa nyumbani kwao Uwanja wa Nangwana Sijaona, Mtwara.
Kibadeni aliingia JKT baada ya timu hiyo kuamua kuachana na Fred Felix Minziro kutokana na mwendo wa kikosi hicho kuwa wa kusuasua.